#Business

WAKULIMA WAKWEPA MIKOPO RASMI- RIPOTI.

Asilimia kubwa ya wakulima nchini sasa wamegeukia mikopo ya benki za biashara na mikopo ya kidigitali na kukwepa mashirika mbali mbali ya uwekezaji kama vile Hazina ya Serikali ya Hustler, benki ndogo za fedha, mashirika ya mikopo, na wakopeshaji wasio rasmi.

 Kufuatia taarifa kwenye vyombo vya Habari kuwa utafiti uliofanya na benki kuu nchini CBK unaonyesha kuwa kufikia Mei mwaka huu, hakuna mkulima aliyehojiwa alikuwa amekopa kutoka shirika la mikopo au taasisi ndogo za fedha, huku sehemu ya wakulima waliokopa kutoka benki ikipanda kutoka asilimia 41 mwezi Machi hadi asilimia 58 huku matumizi ya mikopo ya kidijitali pia ikikua kutoka 2% hadi 8% katika kipindi kama hicho.

Utafiti huo aidha umebainisha kuongezeka kwa utegemezi kwa wanunuzi wa mazao ya shambani na vikundi vya kuweka akiba visivyo rasmi, wakati ukopaji kutoka SACCOs ulishuka kwa kasi kutoka 35% hadi 24%. Wakulima pia wanabadilisha jinsi wanavyotumia mikopo kwani wachache wanatumia kwenye pembejeo na vibarua, huku wengi wakifadhili vifaa na mashine.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

WAKULIMA WAKWEPA MIKOPO RASMI- RIPOTI.

KENYA YAPTA HOLIDEI MPYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *