#Sports

OWINO APIGIA UPATO HARAMBEE STARS

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya Sylvester Owino anasema Harambee Stars iko katika nafasi nzuri zaidi ya kukusanya pointi nyingi zaidi kutoka kwa mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Gambia na Ushelisheli.

Owino ambaye pia alijumuishwa katika kikosi cha Harambee Stars katika kinyang’anyiro cha CHAN kilichomalizika hivi majuzi anasema kiwango cha wachezaji waliochaguliwa kwa mechi za kufuzu kinatosha kutoa ubashiri wa ushindi kwa Gambia.

Timu ya Gambia inajumuisha, miongoni mwa wengine, mchezaji wa Brighton na Hove Albion Yankuba Minter ambaye anacheza katika winga. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anajulikana kwa kasi na uthubutu wake, jambo ambalo linafaa kuwatia wasiwasi mabeki wa Harambee Stars

Chini ya usimamizi wa aliyekuwa kocha mkuu wa Gor Mahia Jonathan McKinstry, Gabon pia itahitaji pointi nyingi zaidi ili kuboresha msimamo wa kundi lao na viwango vya FIFA pia.

Kocha McKinstry anasema anafahamu tishio la timu ya Kenya japo anaamini kila mmoja atapigania pointi tatu.

Kwa sasa, Kenya inakamata nafasi ya 4 katika kundi F ikiwa na pointi 6 baada ya kutoka mara sita na Gambia katika nafasi ya 5, ikiwa na pointi 4 kutoka kwa idadi sawa ya mechi na Kenya.

Gabon bado inaongoza kundi ikifuatiwa na Ivory Coast, huku Burundi ikiwa katika nafasi ya tatu katika kundi hilo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

OWINO APIGIA UPATO HARAMBEE STARS

KIKOSI CHA TIMU YA WAVU CHAZINDULIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *