#Local News

CHELEWA CHELEWA ITAKAYOKUGHARIMU MABILIONI.

Wakenya watalazimika kulipa takribani shilingi bilioni 25.3 kama adhabu kugharamia riba ya madeni ya serikali ambayo yamechelewa kulipwa.

Ni onyo iliyotolewa na mdhibiti wa bajeti ya serikali Margaret Nyakang’o, anayesema madeni ya serikali yaliongezeka kwa shilingi bilioni 9 katika kipindi cha mwaka wa kifedha uliopita pekee.

Nyakang’o amesema wizara ya uchukuzi inaongoza kwa deni la hadi shilingi bilioni 121.8, deni analosema limevutia riba ya shilingi bilioni 21.3, huku deni la wizara ya kawi likivutia riba ya shilingi bilioni 1.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHELEWA CHELEWA ITAKAYOKUGHARIMU MABILIONI.

NPS YAENDELEZA AFYA YA KIAKILI

CHELEWA CHELEWA ITAKAYOKUGHARIMU MABILIONI.

OPERESHENI MAALUM YAAGIZWA JIJINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *