#Local News

WAKAZI KUKWAMISHWA NA MCHEZO

Wakazi wa jiji la Nairobi wametatizika kusafiri kutoka na msongamano wa magari, uliosababishwa na kufungwa kwa baadhi ya barabara ili kuruhusu maandalizi ya mechi ya soka baina ya timu ya taifa Harambee Stars na the Gambia itakayochezwa leo katika uwanja wa Kasarani.

Idara ya trafiki imetangaza kufunga barabara kadhaa, watumiaji ya barabara kuu ya Thika wakishauriwa kutumia barabara ya Ruaka-Baba Dogo- Lucky Summer- Nairorobi River- Hadi, kizuizi kikiwekwa katika eneo la Muthaiga.

Maafisa zaidi wa trafiki wametumwa kuekeleza magari kwenye barabara ya Thika Super Highway ili kudhibiti msongamano.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *