ALVAREZ APIGWA MARUFUKU MIEZI KUMI
Beki wa Athletic Bilbao Yeray Alvarez amepigwa marufuku ya miezi 10 baada ya kupatikana na dawa iliyopigwa marufuku kufuatia pambano la Ligi ya Europa dhidi ya Manchester United msimu uliopita, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA lilisema Jumatatu.
Uchambuzi wa sampuli iliyotolewa na mchezaji huyo baada ya mchezo mwezi Mei “ulifichua uwepo wa Canrenone,” dawa iliyopigwa marufuku na Shirika la Dunia la Kupambana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, UEFA ilisema.
UEFA ilikiri kwamba kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alichukua dawa hiyo “bila hiari”, huku Alvarez akisema kuwa ni dawa aliyokuwa akitumia kukabiliana na upotezaji wa nywele kufuatia matibabu ya saratani ya korodani.
Hiyo ina maana kwamba Alvarez ataweza kurejea uwanjani mwanzoni mwa Aprili mwakani, japo ataruhusiwa kurejea mazoezini na wenzake miezi miwili kabla ya hapo.
Alvarez aligunduliwa na saratani ya tezi dume mnamo 2016 na baada ya matibabu alirudi kucheza mnamo 2017, lakini alipatwa na hali hiyo baadaye mwaka huo, na kurudi tena mnamo 2018.
Kipimo chake chanya kilikuja baada ya Athletic kushindwa 3-0 nyumbani na United katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Europa mnamo Mei 1.
Habari za kufungiwa kwake ni pigo kubwa kwa klabu ya Basque, ambayo itashiriki Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Inakuja baada ya hatua ya kumrejesha beki wa kati wa Uhispania Aymeric Laporte katika klabu hiyo kwa kipindi cha pili kutoka kwa Al-Nassr ya Saudia kushindikana mwishoni mwa dirisha la usajili.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































