GAVANA NDETI AWATIMUA MAAFISA ‘FISADI’
Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti amewasimamisha kazi maafisa 33 wa idara ya kukusanya mapato kwa madai ya kuhusika na ufisadi.
Hatua ya Ndeti inajiri kufuatia ongezeko la hofu kuhusu shughuli za udanganyifu, huku gavana huyo akiapa kusambaratisha shughuli hizo ili kuimarisha utoaji huduma kwa wakazi.
Miongoni mwa hulka za udanganyifu ni madai ya maafisa hao kudanganya kuhusu mapato yaliyokusanywa mbali na utoaji wa risiti ghushi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































