HARAMBEE STARS WAREJEA UWANJANI
Harambee Stars itawakosa mabeki Alphonse Omija na Aboud Omar katika mechi ya leo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ushelisheli.
Haya mi kwa mujibu wa kocha Benni McCarthy .
Katika kikao na wanahabari Jumatatu katika uwanja wa moi Kasarani, McCarthy ameelezea matumaini yake kwamba timu hiyo itajikomboa kutokana na kichapo cha 3-1 dhidi ya Gambia,
Huku Aboud na Omija wakikosekana, McCarthy alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja kama kikosi.
Fowadi Mkenya William Lenkupaye, ambaye anacheza mechi yake ya kwanza kikosini, alisema timu hiyo imemkaribisha kwa furaha.
McCarthy alidokeza kutumia wachezaji wengi wa karibu ili kuimarisha kikosi.
Kocha Mkuu wa Shelisheli Ralph Jean-Louis pia alionya kwamba hawako Kenya kwa ajili ya kukamilisha mechi zao tu, bali kutoa tamko licha ya mwenendo wao mbaya hadi sasa.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































