KESI YA ‘ALIYEMUUA” RAIS YAENDELEA
Kesi ya mwanafunzi wa chuo kikuu David Mokaya anayetuhumiwa na mashtaka ya kulidanganya taifa kwa kuchapisha picha zinazoashiria kifo cha rais William Ruto inaendelea katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi ambako mshtakiwa alikana mashtaka.
Mwanafunzi huyo anadaiwa kuchapisha picha ya jeneza lenya bendera ya taifa na maandishi yanayoashiria mazishi ya rais, madai ambayo mawakili wanaomwakilisha wakiongozwa na Danstan Omari wamepinga.
Aidha, mawakili wamesema polisi walikiuka sheria katika kumkamata Mokaya jijini Eldoret ambako walinasa simu na tarakilishi yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































