MSAKO WAIMARISHWA NAIROBI
Washukiwa wa wizi wa kimabavu zaidi ya 300 jijini Nairobi ambao wamekamatwa kufikia sasa wanatarajiwa mahakamani hii leo kufunguliwa mashtaka mbali mbali, baada ya kukamatwa wakati wa operesheni maalum iliyoagizwa na serikali.
Polisi wamewataka waathiriwa wa uhalifu huo katikati mwa jiji la Nairobi kuandikisha taarifa ili kusaidia katika uchunguzi na kufanikisha mashtaka dhidi ya washukiwa.
Wakati uo huo, gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, amewahakikishia wakazi usalama kwa ushirikiano na polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































