#Business

REHANI YA MIRADI YAPIGWA JEKI

Hatua ya serikali kuweka rehani malipo ya baadaye kupitia hazina ya matozo ya utumiaji wa barabara yaani road maintenance levy imepigwa jeki ya shilingi bilioni 16.38 kutoka kwa benki ya UBA.

Mpango huo uliozinduliwa na bodi ya barabara nchini KRB, unalenga kupata fedha za kukusaanya fedha za kufadhili ukarabati wa barabara, kuongeza fedha za kuwalipa wanakandarasi mbali na kupunguza shinikizo kwa serikali huku miradi ikitekelezwa kwa haraka.

Chini ya mpango huo, mikopo inayochukuliwa inalengwa kulipwa kutokana faida za mradi unaofadhiliwa.

KRB ni taasisi ya kwanza nchini inayosimamia miundomsingi ya umma kukumbatia mfumo huo maarufu kama securitization, ambako shilingi 12 kati ya 25 zinazotozwa kwa kila lita ya petroli, zitatumika kulipia mikopo hiyo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

REHANI YA MIRADI YAPIGWA JEKI

KODI YATAJWA KUWA KIZINGITI KWA MAENDELEO

REHANI YA MIRADI YAPIGWA JEKI

PROFESA MUTUA: POKEENI FIDIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *