#Local News

UTAFITI WAFICHUA HALI YA UCHUMI NCHINI

Asilimia kubwa ya wakenya imeripoti kwamba hali yao ya kiuchumi inaendelea kudorora kwa kiwango kikubwa tangu serikali ya Kenya Kwanza ilipoingia madarakani.

Haya ni kwa mujibu wa utafiti wa shirika la TIFA, ulioendeshwa kati ya mwezi jana na mwezi huu, na kulinganishwa na matokeo ya utafiti sawa na huo wa mwezi Mei, ukionyesha kudorora kwa uchumi.

Kwenye utafiti huo, asilimia 64 ya wakenya wanaripoti kudorora kwa uchumi, ikilinganishwa na asilimia 54 ya mwezi Mei, huku walioripoti kuimarika kwa uchumi wao wakipungua kutoka asilimia 29 mwezi Mei hadi asilimia 24.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UTAFITI WAFICHUA HALI YA UCHUMI NCHINI

KODI YATAJWA KUWA KIZINGITI KWA MAENDELEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *