DABI YA MANCHESTER
Na hatimaye baada ya likizo ya kimataifa kwa ligi kuu ya uingereza wafuasi wa ligii hii wanasubiria weekend hii kwa mvuto mkubwa wakisubiria vilabu wanavyo enzi.
Lakini mchezo mkubwa mabao unasubiriwa ni kati wa miamba wa wawili Manchester United na Manchester City almaarufu kama manchester derby jumapili hii katiaka uwanja wa etihad.
Miamba hawa Wawili wanakutana ana kw ana huku wote wakijivunia wingi wa vikombe kati yao na mameneja wawili wa kiwango cha kimataifa.
Kukiwa na ushindani mkali, kumekuwa na mchuano mkali kati ya pande hizo mbili za Manchester siku za nyuma.
Mkutano wa kwanza kati ya timu hizo mbili ulifanyika tarehe 12 Novemba 1881, wakati West Gorton, ambaye baadaye illitwa Manchester City – ilikaribisha Newton Heath, ambaye baadaye iliitwa Manchester United ambapo Mchezo ulimalizika kwa 3-0 kwa upande wa Newton Heath yani manchestro united
Wawili hao wakawa timu zilizotawala katika eneo la Manchester; mshindi wa Kombe la Manchester alikuwa ama Newton Heath au Ardwick kila mwaka kati ya 1888 na 1893.
Kiingilio kwenye Ligi ya Soka hatimaye kilikuja mnamo 1892, wakati Newton Heath alipojiunga na Divisheni ya Kwanza, na Ardwick akajiunga na Divisheni mpya ya Pili.
Pande hizo mbili zimecheza kwa jumla ya mara 189 . Hii imekuwa katika mashindano yote na inajumuisha Ligi Kuu, Daraja la Kwanza, Kombe la FA, Ngao ya Jamii na Kombe la Ligi.
Manchester United wameshinda zaidi ya Manchester City. United wameshinda mara 78, huku City wakiwa wameshinda 58. Kumekuwa na sare 53 kati ya pande hizo mbili.
Je weekend hii nani atanghuruma? Nani atakua simba wa manchester ? yote tisa mpira hudunda kwa dakika tisini .
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































