SHA IMEVUNJA REKODI YA NHIF, MWANGANGI
Shilingi bilioni 70 zimekusanywa chini ya mamlaka ya afya ya jamii SHA tangu kuanzishwa kwake, ikilinganishwa na shilingi bilioni 45 zilizokusanywa katika muda wote wa bima ya zamani ya afya NHIF.
Haya ni kulingana na afisa mkuu mtendaji wa SHA Dakta Mercy Mwangangi, akihojiwa na runinga moja nchini ambako ameweka wazi kwamba shilingi bilioni 8 zimekusanywa chini ya afya ya msingi, bilioni 5.9 kupitia mpango wa matibabu ya dharura nazo bilioni 54 kupitia bima ya SHIF.
Aidha, amesema idara ya DCI inachunguza madai ya udanganyifu wa hospitali zinazolenga kuilaghai mamlaka hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































