#Business

NAIROBI MIONGONI MWA KAUNTI ZILIZOORODHESHWA KWA MATUMIZI KUPITA KIASI YA USAFIRI

Serikali za kaunti zinakabiliwa na kuchunguzwa kwa matumizi ya kupita kiasi katika safari zisizo muhimu. Ripoti ya Mdhibiti wa Bajeti, Margaret Nyakang’o, ilifichua kuwa kaunti 23 kati ya 47 zilishindwa kufikia kiwango cha asilimia 30 ya matumizi ya maendeleo na kutumia mabilioni ya pesa kwa safari za kifahari.

Kama ilivyoripotiwa na afisi ya mdhibiti wa bajeti, Kaunti ya Nairobi inaongoza kundi hilo, huku shilingi milioni 863 zikitumika kwa usafiri, huku afisa mmoja akitumia shilingi milioni 17 kwa safari ya Dubai. Kaunti za Machakos na Kisumu zinafuata, na matumizi ya shilingi milioni 631 na shilingi milioni 491, mtawalia.

Pesa hizo zilitumika kwa safari za kuzuru nchi kama vile Dubai, Uingereza, na Marekani kwa shughuli kama vile mikutano na ziara za mafunzo. Hata hivyo imebainika kuwa kaunti zilizotumia pesa kidogo zaidi katika maendeleo ndizo zilizotumia pesa nyingi katika usafiri.

Imetayarishwa na Mourine Amwayi

NAIROBI MIONGONI MWA KAUNTI ZILIZOORODHESHWA KWA MATUMIZI KUPITA KIASI YA USAFIRI

BARCELONA YAKABA KOO NEWCASTLE

NAIROBI MIONGONI MWA KAUNTI ZILIZOORODHESHWA KWA MATUMIZI KUPITA KIASI YA USAFIRI

WAKENYA MILIONI 2.2 KUTIBIWA BURE, RAIS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *