RUTO: KUNA UBAGUZI KATIKA MSAADA HAITI
Utepetevu wa mataifa na ukosefu wa kujitolea kutimiza ahadi za kurejesha utulivu nchini Haiti ndicho kikwazo kikubwa katika kufanikisha operesheni hiyo inayoongozwa na polisi wa Kenya.
Ndiyo kauli ya Rais William Ruto akizungumza nchini Marekani, ambapo ameyalaumu kutokana na alichokitaja kuwa kurejesha nyuma harakati za kuleta amani katika taifa hilo la Karibia.
Hata hivyo, amekariri kuwa Kenya itasalia nchini humo hadi amani itakaporejeshwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































