#Local News

MUSYOKA ATAKA POLISI WAONDOLEWE HAITI

Ni wakati wa serikali ya Kenya kukiri kwamba imelemewa na operesheni ya kurejesha utulivu nchini Haiti na kuwarejesha nchini maafisa wake wa polisi.

Ni kauli ya kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, ambaye amekosoa serikali kwa madai ya kupotoshwa kuhusiana na kuwatuma maafisa wake nchini humo, hasa baada ya kubainika kuwa maafisa 3 wamefariki kufikia sasa.

Usemi wa Musyoka unajiri baada ya Rais William Ruto kuyashutumu mataifa anayosema yalikosa kutimiza ahadi zake kuhusiana na operesheni hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MUSYOKA ATAKA POLISI WAONDOLEWE HAITI

ODM YAMTEUA MWANIAJI WA UBUNGE KASIPUL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *