NSL YAPATA UDHAMINI
Wimbi la matumaini linazidi kutanda katika Ligi Kuu ya Kitaifa (NSL) baada ya kupata udhamini wa Ksh 18 milioni siku chache kabla ya msimu wa 2025-26 kuanza wikendi hii, Septemba 27-28.
Mkataba huo, ambao unaelekeza Ksh5 milioni kwa kila klabu kati ya tatu—3K FC, Kisumu All Stars, na Migori Youth—pamoja na Ksh1 milioni za bidhaa, umeibua hisia za shauku kutoka kwa viongozi wa klabu na viongozi wa soka wanaotamani kuona ligi ikifungua ukurasa mpya.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kisumu All Stars Nicholas Ochieng akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo, aliutaja ushirikiano huo kuwa wa mafanikio
Msimu unapoanza, 3K FC, Kisumu All Stars, na Migori Youth wanaamini kuwa udhamini huu unaweza kuamsha ndoto zao za kukuza na kuweka kiwango kipya cha ukuaji wa ligi.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































