POLISI WAANZA MSAKO DHIDI YA WALIOKOSEA HESHIMA BENDERA
Tukio la vijana wawili raia wa Somalia kuidhihaki bendera ya Kenya wakati wa mechi ya soka katika uwanja wa Nyayo wikendi iliyopita limechukua mkondo wa kidiplomasia, ubalozi wa Somalia humu nchini ukilazimika kuomba msamaha.
Kwenye tukio hilo ambalo limetawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii, vijana hao walinaswa kwenye video wakiikanyaga bendera ya Kenya na kuirusha kiholela, hatua ambayo imesababisha Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen kuagiza kukamatwa, kushtakiwa na kufurushwa kwa wahusika.
Idara ya polisi imethibitisha kuanza msako dhidi ya raia hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































