#Local News

IEBC TAYARI KWA USAJILI, MWENYEKITI

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imeweka mikakati jumuishi itakayohakikisha usajili wa juu zaidi wa vijana kama wapiga kura kwenye usajili utakaofunguliwa Jumatatu ijayo.

Ni hakikisho la mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon, akizungumza alipofika mbele ya kamati ya utekelezaji wa katiba bungeni, akisema tume hiyo inalenga kuwasajili wapiga kura wapya hasa vijana milioni 6.3 katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Aidha, amevitaka vyama vya kisiasa kuhakikisha mchujo unafanywa kwa njia huru bila vurugu jinsi ilivyoshuhudiwa katika eneo bunge la Kasipul Jumatano.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

IEBC TAYARI KWA USAJILI, MWENYEKITI

KAWU: MGOMO WETU BADO UPO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *