#Local News

MSHTUKO KERICHO, JAMAA AWAUA WATU 3

Wakazi wa Kijiji cha Samutet kaunti ya Kericho wameachwa na mshtuko baada ya mwanamme mwenye umri wa miaka 19 kuripotiwa kuwaua kwa kuwakatakata watu 3 ambao ni shangazi yake, shemeji yake na mpwa wake kutokana na sababu ambazo hazijajulikana.

Kamanda wa polisi kaunti hiyo James Ng’etich amesema mshukiwa kwa jina Evans Kiprop alianza kwa kumshambulia shangazi yake mwenye umri wa miaka 70, kabla ya kumgeukia shemeji yake mwenye umri wa miaka 28 na mpwa wake mwenye umri wa miaka 3 kwa panga.

Ameongeza kuwa mshukiwa ambaye ana rekodi ya uhalifu, aliteketezwa na wakazi wenye hamaki.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MSHTUKO KERICHO, JAMAA AWAUA WATU 3

KIKOSI CHA BASEBALL CHAINGIA HATUA YA ROBO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *