UHURU: UONGOZI HAUHITAJI UCHUNGU, HASIRA AU CHUKI
Rais wa zamani Uhuru Kenyatta amesema kwamba katika siasa, kiongozi hawezi kuongozwa na uchungu, hasira au chuki.
Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Chama cha Jubilee, Kenyatta amesema siasa inapaswa kuwa chombo cha kuleta umoja na maendeleo kwa wananchi, badala ya kugawanya watu kwa misingi ya tofauti za kisiasa.
Kenyatta amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuweka mbele maslahi ya taifa na kujiepusha na misukumo ya kibinafsi inayoweza kusababisha uhasama na migawanyiko.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































