IEBC YAANZA USAJILI WA WAPIGA KURA
Zoezi la kuwasajili wapiga kura zaidi linafunguliwa rasmi hii leo, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikisema inalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni 6.3 katika zoezi hilo.
Wanaosajiliwa ni wakenya walio na umri wa miaka 18 au zaidi, zoezi hilo likiendeshwa katika vituo vya huduma yaani Huduma Centers na afisi za usajili za IEBC kote nchini.
Wakati uo huo, viongozi kutoka serikalini na upinzani wamewarai wakenya kukumbatia fursa hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































