MAKURUTU WA POLISI KUJUA HATMA LEO
Idara ya polisi imeratibiwa kutoa taarifa kuhusu zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na idara hiyo kufuatia kikao cha wakuu wa usalama kitakachoandaliwa katika chuo cha kutoa mafunzo ya polisi mtaani Embakasi hii leo.
Wakuu hao wa usalama watatoa taarifa ya Pamoja baada ya kikao cha Pamoja, ili kutoa mwelekeo kuhusu usajili wa makurutu ambao umekumbwa umecheleweshwa kutokana na mvutano kati ya idara ya huduma kwa polisi NPS na tume ya kutoa huduma kwa polisi NPSC.
Jumla ya makurutu 10,000 wanalengwa kusajili kujiunga na vikosi mbali mbali vya polisi.
Imetayarishwa na Antonty Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































