ROBO TATU YA KAMPUNI NCHINI ZASHINDWA KULIPA KODI
Ni pigo kwa mamlaka ya ushuru KRA baada ya takwimu za mwaka wa kifedha unaoisha Juni 2025, kuonyesha kuwa kampuni 156,232 pekee zililipa ushuru wa mapato ya shirika (CIT), ikiwa ni asilimia 25.2 ya kampuni zote zinazofanya kazi nchini.
Kulingana na ripoti kutoka mamalaka hiyo, kampuni 461,969 kati ya kampuni 618,201 zilizosajiliwa zilishindwa kutimiza majukumu yao ya ushuru licha ya dhuluma kali za ushuru.
Wataalamu wakizungumza na wanahabari wamesema kuwa kushindwa kutuma ushuru kunapita zaidi ya hasara inayoletwa na kampuni mbali mbali na hali ya uchumi. Stephen Waweru, meneja mkuu wa huduma za ushuru wa KPMG, amebainisha kuwa ingawa kampuni nyingi zinawasilisha marejesho ya kodi, ni wachache wanaolipa kodi hiyo – akitaja kuwa sehemu kubwa ya kampuni zinapata hasara. Hii inaweza kusababishwa na mfumuko mkubwa wa bei, mabadiliko ya sarafu, na kupanda kwa gharama za pembejeo.
Baadhi ya kampuni, ingawa zimesajiliwa na kushikilia nambari za PIN, husalia tuli, na kuzifanya zishindwe kutuma kodi. Wengi mara nyingi husajiliwa ili kusambaza bidhaa kwa mashirika ya serikali pekee.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































