KENYA YAZIHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUUNDA UTALII UNAOSTAHIMILI HALI YA HEWA
Naibu Rais Kithure Kindiki ametoa wito kwa nchi za Afrika kuwa na bidhaa anuai za utalii ambazo ni endelevu na zinazostahimili misukosuko ya nje, ikiwemo hali ya suitofahamu ya kijiografia na ushindani mkali kutoka maeneo mengine.
Wito umetolewa alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 15 ya Utalii ya Magical Kenya jijini Nairobi, ambapo amesema soko la utalii la Afrika lina fursa za ukuaji endelevu kama litaungwa mkono na sera wezeshi na mazingira ya udhibiti.
Aidha Kindiki amebainisha kuwa Afrika imeibuka kuwa mojawapo ya kanda zilizofanya vizuri katika kufufua utalii duniani mwaka 2025, akiongeza kuwa bara hili lazima liongeze ubunifu ili kuimarisha ustahimilivu wa sekta hiyo.
Kenya ni mwenyeji wa maonesho hayo ya siku tatu yanayomalizika leo hii, ambayo yamevutia wajumbe 6,500 kutoka mataifa 40, wakiwemo mawaziri wa utalii, mameya wa miji, wawekezaji, watu wanaopenda kusafiri na watangazaji.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































