PVK YAWAHIMIZA WAKENYA KUJISAJILI KAMA WAPIGA KURA
Mwenyekiti wa muungano wa Pentecostal Voice of Kenya PVK Apostle Peter Manyuru, amewahimiza wakenya kujisajili kwa wingi kama wapiga kura kwenye zoezi linaloendelea kote nchini.
Akizungumza baada ya kuongoza mkutano wa viongozi wa muungano huo, Apostle Manyuru ambaye pia ni kiongozi wa kanisa la JTM, amesisitiza kuwa hiyo ndiyo njia mwafaka ya kuwachagua viongozi watakaoleta mabadiliko nchini.
Aidha, ameitaka serikali kuangazia suala la ufisadi katika mamlaka ya afya ya jamii SHA ili kuwaondolea wakenya mahangaiko.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































