FIDIA YA MAANDAMANO: MAHAKAMA YAZUIA JOPOKAZI, TENA
Mahakama kuu mjini Kerugoya imeongeza agizo linaloifutilia mbali utendakazi wa jopokazi lililoteuliwa na rais William Ruto kuweka mfumo wa kuwafidia waathiriwa wa maandamana na ghasia zilizotokea wakati wa maandamano.
Hakimu Edward Muriithi ametoa uamuzi wa kuzuia utendakazi wa jopokazi hilo ukisubiri malalamishi ya wahusika katika kesi hiyo yatakaposikilizwa tarehe 21 mwezi huu.
Uamuzi huo unajiri huku rais wa LSK Faith Odhiambo akijiuzulu kutoka wadhifa wa naibu mwenyekiti wa jopokazi hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































