#Business

KENYA YALENGA KUPATA MAUZO ZAIDI YA NJE KUPITIA EU NA COMESA

Serikali kuu iko mbioni kuongeza juhudi za kufufua mauzo ya nje ya kilimo hadi Ulaya na hata katika masoko mapya ya Afrika kwa kuoanisha viwango vya bidhaa, kuondoa vizuizi visivyo vya ushuru, na kuboresha usafiri wa kikanda.

Waziri wa Biashara Lee Kinyanjui, akizungumza katika Kongamano la COMESA Horticulture Connect jijini Nairobi, aMEsema serikali inashirikiana na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Umoja wa Ulaya (EU) ili kuimarisha upatikanaji wa soko la mauzo ya bustani nje ya nchi, ambayo ni chanzo kikuu cha fedha za kigeni licha ya kupungua kwa hivi karibuni.

Wakati huo huo Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe amesema Kenya tayari imepiga marufuku dawa za kuua wadudu Zaidi 200 ambazo hazifikii viwango vya kimataifa na inafanya kazi na washirika wa kanda kuoanisha hatua za usafi wa mazingira kote COMESA ili kurahisisha biashara ya mipakani.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *