DCP YATETEA UAMUZI WAKE MALAVA
Chama cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kimetetea uamuzi wake wa kumwasilisha mgombeaji kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika eneo la Malava Edgar Busiega, licha pingamizi kutoka kwa chama tanzu cha muungano wa upinzani DAP-K.
Naibu kinara wa DCP Cleophas Malala, amesema uamuzi huo hautishii umoja wa upinzani, anaosema utasalia imara kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao.
Amekariri kuwa hatua hiyo ni ishara ya DCP kukuza demokrasia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































