#Sports

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KUAGA

Timu ya taifa Harambee Stars inajiandaa kwa mechi yao ya mwisho dhidi ya Ivory Coast Jumanne wiki ijayo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burundi hapo jana kwenye mechi za kuwania kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao.

Mshambulizi wa klabu ya Wolfsberger Ryan Ogam aliyeingia kama nguvu mpya, aliifungia Stars bao la pekee la mchezo katika uwanja wa Intwari jijini Bujumbura Burundi na kuhakikisha kuwa Stars wanayaaga mashindano kwa fahari.

Kipa wa Harambee Stars Brian Bwire alilazimika kuondoka mchezoni kunako dakika ya kwanza baada ya kugongana na fowadi wa Burundi Caleb Benyimana, tukio lililosababisha refa kutoa kadi nyekundu na kuilazimu Burundi kucheza wakiwa 10 kwa zaidi ya dakika 90.

Licha kuwa chini, safu ya mashambulizi ya Kenya ikiongozwa na Michael Olunga na kiungo Austin Odhiambo ilifeli kuitishia safu ya ulinzi ya Burundi, na badala yake Burundi wakiongozwa na Jean Claude Girumugisha ikiisumbua safu ya ulinzi ya Kenya mara kwa mara.

Ushindi huo ni wa pili kwa Kenya katika mashindano hayo chini ya kocha Benni McCarthy, ambaye anasisitiza kujenga kikosi kikubwa na kukipa fikra za ushindi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KUAGA

DCP YATETEA UAMUZI WAKE MALAVA

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KUAGA

KIZAAZAA CHA TIKETI KUNDI C

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *