“HASARA YA UKOSEFU WA CHAKULA CHA GMO”
Kenya imepoteza zaidi ya Ksh.20 bilioni katika kipindi cha miaka mitano pekee kutokana na kucheleweshwa kwa kuidhinisha aina za hali ya juu za mazao ya GMO ambazo zinaweza kuimarisha usalama wa chakula na mapato ya wakulima.
Ripoti mpya inaonya kwamba habari potofu na vikwazo vya udhibiti vinaweka teknolojia zinazobadilisha maisha kutoka kwa mikono ya wakulima na hivyo kugharimu mabilioni ya nchi.
Utafiti huo ambao umepewa jina la ‘The Cost of Delay’ unatoa taswira ya kustaajabisha ya kile ambacho Kenya inapoteza kwa kutotumia aina tatu za juu za mazao ambazo ni mahindi na pamba yanayostahimili wadudu, na viazi vinavyostahimili ugonjwa wa blight.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































