IEBC YAKAMILISHA UIDHINISHAJI WAKE
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imekamilisha zoezi la kuwaidhinisha wagombeaji wa chaguzi ndogo za Novemba 27 katika maeneo yote 24 nchini, na kupisha rasmi kipindi cha kampeni kwa wagombeaji kusaka uungwaji mkono wa wapiga kura.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, amesema tume hiyo imetenga muda wa siku 10 kushughulikia mgigogoro yoyote za uteuzi, huku akiagiza kwamba kampeni zitasitishwa saa 48 kabla ya uchaguzi kufanywa.
Naye naibu wake Fahima Arafat, amewatahadharisha maafisa wa usalama na wale wa IEBC dhidi ya kuchukua miegemeo ya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































