#Sports

KIZAAZAA CHA TIKETI KUNDI C

Katika mechi za kufuzu mashindano ya kombe la dunia mwaka ujao, kizaazaa kinatarajiwa katika kundi C wakati Benin walio na alama sawa na South Africa, watakuwa ugenini dhidi ya Rwanda hii leo, siku ambayo pia South Africa watakuwa ugenini dhidi ya Zimbabwe.

Nigeria ambao pia wana nafasi ya kufuzu kwa kombe hilo, watashuka dimbani dhidi ya Lesotho.

Nigeria watawakaribisha Benin katika mechi yake ya mwisho Jumanne wiki ijayo, huku Bafana Bafana wa South Africa nao wakitamatisha kampeni yao dhidi ya Rwanda siku iyo hiyo.

Bafana Bafana na Benin wanatoshana alama wote wakiwa na 10, huku Super Eagles wa Nigeria wakifuata kwa karibu na alama 11.

Kiongozi wa kundi baada ya mechi 2 zilizosalia atafuzu moja kwa moja kushiriki kombe la dunia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KIZAAZAA CHA TIKETI KUNDI C

HARAMBEE STARS WAJIANDAA KUAGA

KIZAAZAA CHA TIKETI KUNDI C

SHUJAA IKO TAYARI, NAHODHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *