SHUJAA IKO TAYARI, NAHODHA
Nahodha mwenza wa kikosi cha raga cha Shujaa, George Ooro anaamini kwamba mashindano ya Safari Sevens yatakayofanyika wikendi hii hii yatakuwa maandalizi mazuri kwa michuano ya “Dubai Invitational” mwishoni mwa Novemba mwaka ujao.
Mshambuliaji huyo amesema kuwa timu itajiandaa ipasavyo katika maandalizi, siyo tu kwa ajili ya mashindano ya Dubai, bali pia kwa duru ya pili ya World Seven Series (WSS) inayotarajiwa kufanyika Machi mwaka ujao.
Ooro alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































