BARABARA YA NJORO-MAU SUMMIT KUFUNGWA
Mamlaka ya kitaifa ya barabara kuu nchini imetangaza kufungwa kwa muda barabara ya Njoro- Mau summit ili kupisha kazi muhimu kwa ujenzi wa lami kufanyika .
Kupitia tangazo la umma mamlaka hiyo imesema kuanzia tarehe 16 mwezi huu hadi tarehe 6 mwezi ujao, barabara hiyo itafungwa huku madereva wanaotumia barabara hiyo wakishauriwa kutumia barabara ya Kibunja kama njia mbadala .
Watumiaji wa barabara wametakiwa kufuata maelekezo kutoka kwa mamlaka hiyo ili kuhakikisha kuna usafiri mzuri wakatai wa ujenzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































