TAJI BAADA YA TAJI KWA KIPYEGON
Bingwa mshikilizi wa rekodi ya dunia Faith Kipyegon ameendeleza umahiri wake uwanjani baada ya kunyakua taji lake la pili mfululizo kwenye mashindano ya Tiffany Athlos kwa mwendo wa kasi zaidi kuwahi kukimbiwa nchini Marekani.
Mashindano ya Athlos huwajumuisha wanawake pekee yaliyozinduliwa Septemba mwaka jana jijini New York Marekani.
Kipyegon alishinda mbio za mita 1,500 katika mashindano ya ufunguzi kabla ya kutetea ubingwa wake katika mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Mkenya huyo aliandikisha muda wa dakika 4, sekunde 17.78, mbele ya wanariadha wengine mahiri Gudaf Tsegay wa Ethiopia ambaye ni bingwa mara 3 wa dunia, mkenya Susan Ejore- Sanders na mshikilizi wa rekodi ya Marekani Nikki Hiltz.
Tsegay alimaliza wa pili kwa muda dakika 4 sekunde 19.75 naye Hiltz akimaliza wa 3 katika muda wa dakika 4 sekunde 32.51
Ushindi wa hivi punde wa Kipyegon unarembesha msimu ambao umeweka kama mojawapo ya wanariadha mahiri wa mbio za mwendo wa kati katika historia.
Mapema mwaka huu, alivunja rekodi ya mbio za mita 1,500 katika mbio za Prefontaine Classic kabla ya kuweka rekodi mpya katika Makala ya Paris.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































