DE BRUYNE AIPEPETA UBELGI KILELENI KWA KUNDI
Kiungo wa Napoli Kevin De Bruyne alifunga mara mbili kupitia mikwaju ya penalti na kuiweka timu yake ya taifa ya Ubelgiji katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao, walipopata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Wales.
Ubelgiji wanaonolewa na Rudi Garcia, walijipata nyuma ya Wales katika uwanja wa Cardiff kupitia goli la mapema lake Joe Rodon, ila kiungo huyo wa zamani wa Manchester City akasawazisha mambo dakika ya 18.
Mabao mengine yalifungwa na Thomas Meunier na Leandro Trossard.
Ubelgiji ambao sasa wanaongoza kundi J pointi moja mbele ya North Macedoani, watahitaji ushindi mmoja pekee katika mechi 2 zilizosalia dhidi ya Kazakhstan na Liechtenstein.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































