#Sports

FIFA YAELEZA MATUMAINI MAREKANI ITAKUWA TAYARI

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limesema kwamba lina matumaini kwamba miji 16 itakayoandaa fainali za kombe la dunia nchini Marekani mwaka ujao itakuwa tayari kuandaa mashindano hayo.

Hii ni baada ya kauli ya Rais wa marekani Donald Trump kudokeza kwamba mechi hizo zinaweza kuhamishiwa maeneo mengine kutokana na hofu za kiusalama.

Siku ya Jumanne wiki hii, Trump alisema kwamba atafanya mashauriano na Rais Wa FIFA Gianni Infantino kuhusu kuhamisha mechi za kombe la dunia kutoka miji ya Marekani iwapo italazimika.

Marekani itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia Pamoja na Mexico na Canada.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

FIFA YAELEZA MATUMAINI MAREKANI ITAKUWA TAYARI

STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *