MWILI WA ODINGA WAWASILI JKIA
Ndege ya RAO001 iliyobeba mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA dakika chache zilizopita, siku moja baada ya kifo chake nchini India.
Viongozi mashuhuri wakiongozwa na rais William Ruto, naibu wake Kithure Kindiki, rais mstaafu Uhuru Kenyatta, mawaziri na viongozi wengine wakuu kutoka mirengo yote ya kisiasa wamewasili.
Wakenya wamefika kwa wingi uwanjani humo kupokea mwili wa Odinga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































