#Local News

MWILI WA ODINGA WAWASILISHWA KASARANI

Maelfu ya waomboleza wamefurika katika uwanja wa michezo ya Kasarani jijini Nairobi tayari kutazama mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Mwili huo tayari umewasili uwanjani humo baada ya zaidi ya saa 5 barabarani, maafisa wa jeshi na wale wa polisi wakiwa na wakati mgumu kuwadhibiti waombolezaji kwenye msafara huo ambao umekuwa na viongozi wakuu serikalini akiwemo rais William Ruto.

Kwa sasa kinachosubiriwa ni mwelekeo kuhusu utaratibu wa kuutazama mwili huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWILI WA ODINGA WAWASILISHWA KASARANI

IBADA YA MAZISHI YA ODINGA KUANZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *