#Sports

STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON

Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets imezidisha maandalizi yake ya mchuano kati yao na wenzao wa Gambia katika safari ya kuelekea mashindano ya kombe la wanawake la ubingwa wa bara Afrika WAFCON.

Awamu ya kwanza ya mechi hiyo itaandaliwa Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nyayo, kabla ya marudiano tarehe 28 katika uwanja wa Stade Lat Dior nchini Senegal.

Starlets ambao wamo katika kambi ya mazoezi jijini Nairobi, wameonyesha matumaini ya kuibuka na ushindi, wakisema wako tayari kwa michuano hiyo.

Chini ya uongozi wa kocha wao mkuu Beldine Odemba, Starlets wamekuwa wakinoa makali yao na ushirikiano uwanjani.

Kenya inalenga kurejea katika mashindano ya WAFCON tangu mwaka wa 2016 waliposhiriki kwa mara ya kwanza.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON

FKF YAFUTILIA MBALI LIGI KWA SIKU 7

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *