KABURI LA ODINGA LAANDALIWA BONDO
Maandalizi ya eneo atakakozikwa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga katika eneo la Bondo kaunti ya Siaya yanaendelea, zikiwa ni siku 2 pekee zimesalia kabla ya mazishi hayo.
Shughuli ya uchimbaji kaburi ilianza hapo jana baada ya eneo kutambuliwa na kakake Odinga, Oburu Odinga, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya kitaifa ya mazishi.
Kulingana na Oburu, hafla ya mazishi ya Odinga itakuwa ya faragha, ikihudhuriwa na watu wachache walioteuliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































