WAKENYA WAOMBOLEZA ODINGA NYAYO
Hali ya huzuni imetanda kwa muda katika uwanja wa michezo wa Nyayo, wakenya wakitokwa na machozi wakati mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umewasili kwa ajili ya ibada ya kitaifa ya mazishi.
Baadhi ya waombolezaji walisimama pembeni pa barabara ambako mwili wa Odinga ulipita kutia kutoka majengo ya bunge la kitaifa wakipunga vijibendera
Wamemkumbuka Odinga kwa mchango wake katika demokrasia na ugatuzi.
Imetayarishwa na Antony Nyonyesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































