UEFA KUENDELEA, SIMEONE AKIHOFIA ARSENAL
Kocha mkuu wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amesema kuwa anatarajia pambano kali katika mechi ya ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya watakaposhuka dimbani ugenini dhidi ya Arsenal hii leo.
Akizungumza na wanahabari kabla ya pambano hilo, Simeone ambaye anafahamika kwa mechi za kukaba, amesema klabu yake ina kile alichokitaja kuwa kitambulisho wazi na wataitatiza Arsenal yake Mikel Arteta.
Atletico watategemea huduma za mshambulizi wa Argentina Julian Alvarez, ambaye anarejea Uingereza kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka Manchester City mwaka jana.
Kwa sasa wamecheza mechi 6 bila kupoteza katika mashindano yote, na wanaingia katika mechi ya leo baada ya ushindi wa mabao
5-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt, baada ya kupoteza mechi ya ufunguzi mikononi mwa Liverpool.
Hata hivyo, watakabana koo na Arsenal ambayo haijafungwa bao katika mashindano ya UEFA msimu huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































