#Sports

HAALAND HASHIKIKI TENA

Erling Haaland alifunga mara ya 12 mfululizo jana usiku na kuisaidia klabu yake ya Manchester City kupata ushindi kwa mara ya kwanza ugenini katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kwenye mashindano ya bara Ulaya.

Bao la fowadi huyo raia wa Norway na nahodha Bernado Silva yaliihakikishia City ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Villareal ya Uhispania katika mechi za klabu bingwa barani Ulaya.

Kwa sasa Haaland amefunga mabao 24 katika mechi 14 za klabu na timu yake ya taifa ya Norway msimu huu.

Vijana wa Pep Guardiola walionyesha mchezo mzuri na kutamalaki kipindi cha ufunguzi, mawing’a Jeremy Doku na Savinho wakitatiza safu ya ulinzi ya Villareal mara kwa mara.

Hata hivyo, hofu yao ni jereha kwa kiungo Nico Gonzalez, ambaye ametegemewa pakubwa kujaza pengo la Mhispaniola mwezake Rodri ambaye amesumbuliwa na jeraha la goti la msuli mara kwa mara.

Ushindi huo unaweka katika nafasi ya 5 kwenye jedwali kwa pointi 7, wakiwania kumaliza katika nafasi ya nane bora ili kukwepa awamu ya mwondoano jinsi ilivyofanyika msimu jana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HAALAND HASHIKIKI TENA

GYOKERES AKATA KIU CHA MAGOLI

HAALAND HASHIKIKI TENA

GAVANA KAHIGA AJIUZULU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *