MAGAVANA KUJADILI KAULI ZA KAHIGA
Baraza la magavana limeratibu kikao asubuhi hii kujadili kauli tata za gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga ambazo zimeibua shutuma na mshangao nchini baada ya kuonekana zikisherehekea kifo cha waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Kulingana na kauli za gavana huyo, Odinga ndiye alikuwa akizuia maendeleo kutekelezwa katika eneo la Mlima Kenya, kwa madai kwamba alikuwa akielekeza miradi hiyo katika eneo la Nyanza.
Miongoni mwa yatakayojadiliwa ni uwezekano wa kumpokonya wadhifa wa naibu mwenyekiti wa baraza hilo, huku chama cha UDA kikiarifiwa kuwaagiza wawakilishi wadi kwenye kaunti hiyo kuanzisha mchakato wa kumtimua madarakani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































