#Sports

LIVERPOOL WAMEKUNG’UTA VUMBI, CHELSEA NA MADRID WASHINDA

Mshambulizi wa Liverpool Hugo Ekitike alifunga dhidi ya timu yake ya zamani jana usiku Liverpool ilipoweka kando masaibu yao na kuizaba Eintracht Frankfurt mabao 5-1 katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Mabingwa hao watetezi wa EPL waliingia mechezoni wakiwa wamepoteza mechi 4 mfululuzo, kikiwemo kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Galatasaray katika mechi ya kuwania ubingwa huo.

Hata hivyo, walitoka nyuma na kuandikisha ushindi huo dhidi ya Frankfurt, ambao wamepokezwa kichapo cha mabao 5-1 mfululizo barani Ulaya, baada ya kuandikisha ushindi wa mabao 5-1 katika mechi yao ya ufunguzi.

 Rasmus Kristensen aliwaweka wenyeji kifua mbele, ila Ekitike akasawazisha dhidi ya klabu aliyoigura mwezi Julai kwa kima cha Uro milioni 79.

Wafungaji wengine walikuwa Virgil van Dijk, Ibrahim Konate, Cody Gakpo na Dominik Szoboszlai

Katika matokeo mengine, Chelsea ilipata ushindi sawa dhidi ya Ajax Amsterdam ugani Stamford Bridge, mabao yakipachikwa wavuni na matineja Marc Guiu, Enzo Fernandez, Willian Estevao, Tyrique George na Moises caicedo, huku Wout Weghorst akifuta machozi Ajax kupitia mkwaju wa penalti.

Wakati uo huo, Baren Munich ni moja kati ya timu tano wakiwemo mabingwa watetezi PSG zilizo na pointi 9 kutokana na mechi 3, baada ya Harry Kane kufunga bao lake la 20 la msimu katika mechi 12 na kuwapa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Club Brugge.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *