#Local News

SENETI YAWATAKA MCAS MAKUENI KUIWAJIBISHA SERIKALI

Kamati ya afya katika bunge la seneti imelitaka bunge la kaunti ya Makueni kuiweka mbioni serikali ya kaunti hiyo ili kuimarisha utoaji wa huduma za kiafya kwa Wakazi wa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya kamati hiyo kuzuru hospitali kadhaa za kaunti hiyo ikiwemo ile ya rufaa mjini Wote na kubaini ilichotaja kama uendeshaji mbaya wa masuala ya afya katika kaunti hiyo.

Wakiongozwa na seneta wa Bungoma Wafula Wakoli, maseneta hao wameibua masuala kadhaa ikiwemo wahudumu wa afya ya nyanjani CHPs kukosa kulipwa mishahara yao kwa miezi kadhaa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SENETI YAWATAKA MCAS MAKUENI KUIWAJIBISHA SERIKALI

RUTO ATETEA SHERIA ZA MITANDAO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *