#Football #Sports

VINICIUS AOMBA RADHI KWA MASHABIKI

Winga wa Real Madrid, Vinicius Junior, ameomba radhi kwa
mashabiki kufuatia mwenendo wake wakati wa ushindi wa timu
yake 2–1 dhidi ya Barcelona katika mechi ya El Clásico
iliyochezwa Jumapili.
Vinicius alionyesha hasira baada ya kutolewa dakika ya 72 kwa
kuondoka moja kwa moja kuelekea vyumba vya kubadilishia
nguo, kitendo kilichowakera baadhi ya mashabiki.
Hata hivyo, baadaye alirejea kwenye benchi na baada ya mechi,
alionekana akijaribu kumkabili mchezaji wa Barcelona Lamine
Yamal, hali iliyozua tafrani uwanjani Santiago Barnebeu
Mchezaji huyo wa Raia Wa Brazil amesema anajutia matendo
yake na ameahidi kudhibiti hisia zake katika mechi zijazo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *