#Football #Sports

GUARDIOLA  ALAUMU WAAMUZI WA EPL

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amewashambulia
waamuzi wa Ligi Kuu ya Uingereza, akidai kuwa amekuwa
akikumbwa na maamuzi yenye utata kwa kipindi cha miaka kumi
bila kupata maelezo ya kuridhisha kutoka kwao.
Guardiola alionekana mwenye hasira baada ya mwamuzi
Anthony Taylor na timu yake – ikiwemo wale wa VAR –
kuruhusu bao la Tyler Adams wa Bournemouth kusimama
wakati wa mechi ya Jumapili iliyochezewa Etihad Stadium, licha
ya City kulalamikia ukiukaji wa sheria katika mchakato wa bao
hilo.
Kocha huyo wa Uhispania alisema hatarajii waamuzi hao
kujitokeza kueleza maamuzi yao, akisisitiza kuwa hali hiyo
imekuwa ikijirudia mara kwa mara katika mechi za timu yake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

GUARDIOLA  ALAUMU WAAMUZI WA EPL

HARRY KANE AVUTIWA NA BARCELONA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *